Wengi Wamelalamika kwa Sababu Wasanii Wengi akiwemo Diamond,Chege,Temba,Madee,Afande Sele na Wengine Kibao hawajafanya show Wakati walikuepo kwa Ratiba.Kama Vile
haitoshi hata Msanii kutoka Sweden Mahombi hajafanikiwa kufanya show.Watu wamesubiri mpaka saa 11 alfajiri hatimaye wakakata tamaa na kuanza kuondoka huku lawama nyingi zikienda kwa Waandaaji kwa kutojipanga Vizuri.
Watu kiukweli walijaa sana na wamepata adhabu ya kusimama zaidi ya Masaa 10 kwa sababu kulikuwa hakuna Viti wala mahali pa kukaa hivyo ukiingia ndani ni kusimama mpaka show inaisha.
Kitu kingine kibaya ni kujaa kwa Wauni wengi nje ya ukumbi nawatu wameporwa vitu vyao hadharani tena kwa nguvu.
Maoni yangu kwa Waandaaji ni kujipanga ili kuepushana na Aibu waloipata Mwaka huu!!
No comments:
Post a Comment